Kujua zaidi kuhusu historia, dira, maono na muundo wa Shule ya Sekondari ya Mpendae
Shule ya Sekondari ya Mpendae iko kiasi ya kilomita tano (5) kutoka katikati ya mji wa Zanzibar. Ipo wilaya ya mjini katika mkoa wa mjini magharibi. Skuli hii imejengwa kwa mkopo wa Benki ya Dunia na ipo katika mtaa wa Mpendae, katika shehia ya Mpendae.
Shule ya Mpendae ni ya ghorofa moja ambayo iko chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali. Tunajivunia kutoa elimu bora kwa vijana wetu na kuwaandaa kwa maisha ya baadaye.
Shule ya Sekondari ya Mpendae ilianza rasmi tarehe 15 Agosti 2013, wanafunzi wa kidato cha tano waliripoti na kuanza masomo yao. Shule ilianza na jumla ya wanafunzi 61 wa kidato cha tano. Kati yao, 33 walikuwa wa Sayansi na 28 wa Sanaa (Arts).
Mwalimu Mkuu wa kwanza wa shule alikuwa Bwana Mbarouk Habibu Rashid ambaye alisimamia mwanzo wa shule na kuweka misingi imara ya utendaji.
Bwana Mussa Abdi Khamis alichukua nafasi ya Mwalimu Mkuu na kusimamia ukuaji na maendeleo ya shule kwa kipindi cha miaka sita.
Bi. Chausiku M. Panju ni Mwalimu Mkuu wa sasa anayeongoza shule na kuendelea na dira ya kutoa elimu bora kwa vijana wa Zanzibar.
Tangu kuanzishwa kwake, shule yetu imesimamwa na viongozi wenye uzoefu na weledi
Shule ya Mpendae inafanya kazi chini ya muundo ulio wazi na wa kidemokrasia kulingana na kanuni za Wizara ya Elimu
Kamati ya Shule ni chombo kikuu cha maamuzi katika shule kulingana na kanuni na taratibu za Wizara. Kamati hii inaweka sera na mwelekeo wa kimkakati wa shule.
Chini ya kamati, shughuli za kila siku zinasimamwa na Mwalimu Mkuu na timu yake ya usimamizi